Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewatoa hofu Watu ambao watakuwa hawajasajili laini zao kwa alama za vidole hadi kufikia January 20 kwamba licha ya kwamba laini zao zitafungiwa lakini usajili huo ni endelevu.
“Watakaositishiwa huduma za laini zao January 20 wanaweza pia kuendea na utaratibu wa usajili kwa kutumia kitambulisho cha Taifa ili kurudisha laini zao zitakazokuwa zimefungwa au kupata laini mpya, zoezi hili ni endelevu” – TCRA