Muwakilishi wa LaLiga kwa Tanzania na Rwanda Mr Alvaro Paya leo aliratibu mkutano wa online wa waandishi wa habari wa Tanzania kuhusuiana na LaLiga “LaLiga Online Press Conference “
Mkutano huo wa Online ambaye Rama Mwelondo wa AyoTV/millardayo.com alikuwa sehemu ya waandishi wa habari walioshiriki, alipata wasaa wa kupata ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo kumuhoji maswali balozi wa LaLiga na mchezaji wa zamani wa West Ham, Tottenham na Sevilla Frédéric Kanoute.
Kwa upande wa Alvaro Paya alitolea ufafanuzi suala la LaLiga na Yanga kuingia mkataba wa miaka mitatu ni kuwa faida kubwa klabu hiyo itakayoipata ni kubadili mfumo na kuifanya Yanga SC kuwa Proffesional Football Club mfumo ambao utaipa nafasi ya kutengeneza vyanzo vyake vya mapato na kutumia mashabiki wake kama mtaji wake.
Kanouté ameeleza kuwa Samatta ni moja kati ya wachezaji wa Tanzania anaowafahamu na anavutiwa na kukubali kiwango cha mchezaji huyo, LaLiga inatarajiwa kurudi June 11 kwa mchezo kati ya Sevilla dhidi ya Real Betis baada ya mapumziko ya Corona.