Mpango wa 1 wa SADC Live Your Dream Road Tour and Moving Arts (The Great African Art Banner Iniative), safari ya kipekee ya kitamaduni na Sanaa kutoka Tanzania hadi Zimbabwe, inayojumuisha zaidi ya kilomita 6,000 itakayo wapa washiriki kuangazia mandhari mbalimbali za kuvutia unaotarajiwa kuanza hivi karibuni sasa wanukia Kimataifa.
Katika kuelekea safari ya utalii miongoni mwa nchi barani Afrika unaoandaliwa na makampuni ya utalii ikiwemo UPL SAFARI, Origin Trails, Landrover Club Tanzania, Afrika Speaks, The Great African Art Banner inative, Cycle 4 SDGs SADC imefanya ziara fupi iliyowakutanisha na wahisani na viongozi wawakilishi wa nchi za SADC ikiwemo balozi wa Tanzania nchini Malawi Mh.Agness Kayola na kuelezea faida ,umuhimu wa mpango huu unaolenga kutangaza utalii wa nchi ya Malawi kama moja ya nchi iliyo na vivutio vingi ikiwemo utalii wa kuendesha baiskeli.
Kwa upande wake H.E balozi Kayola ametoa pongezi kwa waandaaji wa safari hii ya kihistoria itakayo pitia nchini Malawi,na kupongeza umoja uliooneshwa na nchi ya Tanzania kwa kushirikiana na Zimbabwe ambayo ndio aliyepokea kijiti cha Urais wa SADC kwa mwaka 2024 na kuahidi ushirikiano katika kufanikisha msafara huu wa kihistoria
Pia kamati ilifanikiwa kufanya mkutano na ubalozi wa zimbabwe nchini Malawi na kukutana na Naibu balozi Mh. Matemera akimuwakilisha balozi Mh.Dky Nancy Sanguweme nafasi adhimu ya kuonyesha mipango ya Live Your Dream Road Tour, The Great African Art Banner (GAAB), Africa Day kupanda Mlima Kilimanjaro, Maonyesho ya sanaa na Cycle 4 SDGs SADC na baadae ubalozi uliweza kuchangia mafuta kama moja ya kuonesha mwanzo mzuri utakaodumu wa ushirikiano katika safari hii ya kihistoria
Ziara hiyo inahusisha msafara wa Land Rover 17, zikiashiria nchi 16 wanachama wa SADC na Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).
Malengo makuu ya mpango huu ni Kukuza nchi jumuiya SADC, mawazo, maono, ndoto, vipaji, ubunifu, utalii na biashara kuwahamasisha na kuwatia moyo vijana kufuata na Kuishi ndoto zao
Safari hii itaanzia nchini Tanzania, Malawi, Zambia na katamatika nchini Zimbabwe