Hapa nimekusogezea nukuu za Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango.
“Asilimia 26 ya Watanzania wanaishi chini ya kiwango cha umasikini. Kwa hesabu rahisi ni Watanzania wasiopungua Milioni 13. Ni wengi mno. Lakini wakati huo huo, Mwenyezi Mungu aliipendelea nchi yetu. Kwanza kwa idadi kubwa ya watu, lakini vile vile kwa rasilimali nyingi”- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango
Tanzania kuna rasilimali za kila aina ikiwemo bandari, kwa hiyo umasikini wa watu wetu asilimia 26 hauendani kabisa na upendeleo mwenyezi Mungu aliotupatia kwa kutupatia rasilimali nyingi’- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango
“Tumeazimia kuwa Taifa letu tulipeleke kuwa Taifa lenye kiwango cha juu na cha kati cha kipato haraka iwezekanavyo ili tuweze kuwatoa hawa wenzetu Milioni 13 kutoka kwenye lindi la umasikini. Hatuwezi kuwatoa kwa kuendelea kukalia rasilimali za nchi bila kuzifanyia kazi”- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango
“Sasa kwa rasilimali ya bandari, naomba tu niwaambie viongozi na Watanzania wenzangu, dunia ya leo imejaa ushindani mkali. Kwa hiyo hapa tuliponapo tuna bandari yetu ya Dar es Salaam lakini pia mmesikia bandari nyingine zilizotunzuguka”- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango
“Jirani yetu Kenya ana bandari kubwa ya Mombasa lakini anaendelea kujenga na nyingine. Jirani zetu Msumbiji, Afrika ya Kusini na nyingine Afrika ya Magharibi. Kwa hiyo maana yake bandari yetu isipokua na tija, biashara inakwenda huko kwingine. Kwa hiyo ni lazima tujizatiti, tupambane kiushindani”- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango