Baada ya mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema kufanya mgomo wa siku tatu mfululizo tangu alipokamatwa na polisi ijumaa iliyopita August 26 2016, aligoma kula akishinikiza kupelekwa mahakamani.
Leo August 29 2016 Mbunge Lema amefikishwa katika mahakama kuu Arusha ambapo amesomewa mashtaka mawili la kwanza likiwa ni kutuma ujumbe wa kuudhi kwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo unaosema ‘karibu Arusha tutakudhibiti kama Arabuni wanavyodhibiti mashoga‘ na la pili ni kutuma ujumbe wa sauti kwenye mitandao unaohamasisha maandamano yasiyokuwa na kibali.
Aidha wakati akisubiri dhamana yake Mbunge Lema amezua taharuki mahakamani hapo baada ya kukataa kwenda magereza kabla ya muda wa mahakama kukamilika.
Hata hivyo hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi anayesikiliza kesi hiyo Desideri Kamugisha amemuachia mtuhumiwa kwa dhamana ambapo kosa la kwanza milioni 10 na kosa la pili shilingi milioni 15.
#UPDATE4 Mbunge Lema aachiwa kwa dhamana ambapo kosa la kwanza milioni 10 na la pili shilingi milioni 15 pic.twitter.com/FmjOuo06tD
— millardayo (@millardayo) August 29, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV AUGUST 26 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI