Kiongozi wa Kanisa la Inuka Uangaze, Nabii na Mtume Boniface Mwamposa amesema kuwa tukio la vifo vya watu 20 lililotokea mjini Moshi, Kilimanjaro katika kongamano lake ni jambo kubwa na anatambua kwamba limewaumiza Watanzania wengi pamoja na serikali.
“Namuachia Mungu yeye mwenyewe asimame, kwa sababu lilikuwa jambo sio dogo, ni zito, limewaumiza Watanzania, serikali imeumia, viongozi wameumia lakini mengi tutayajua hapo mbeleni,” Mwamposa.
Ameitoa kauli hiyo mapema leo asubuhi katika viwanja wa Tanganyika Packers, Kawe jiji Dar es Salaam wakati akielekea kuongoza ibada ya Jumapili ambayo amesema ni ya upako, ya kufunguliwa na kuponywa.
Mbali na kutoa pole kwa Watanzania kuhusu tukio hilo lililotokea, amesema kwamba kwa sasa hatoendelea na makongamano aliyokuwa amepanga kufanya hadi hapo atakapotangaza tena.
“Makongamano mengi nimeyasimamisha kwanza. Tunaomba neema ya Mungu ikapate kusimama na watu, baada hapo ndipo nitaweka ratiba ya makongamano” Mwamposa
“Leo lilikuwa liwe kongamano kubwa la kukanyaga mafuta, kwa sababu ya shida iliyotokea tulisimamisha yote, tunataka utulivu na kumuomba Mungu atupe neema ya kupanga mipango mipya.” Mwamposa
Katika kongamano lake la kukanyaga mafuta lililofanyika katika Uwanja wa Majengo, Moshi, Februari Mosi watu 20 walifariki dunia na wengine 16 kujeruhiwa baada ya kukanyagwa na wenzao wakati wakigombea kukanyaga mafuta ambayo kiongozi huyo aliwaambia yana upako.
Februari 4 mwaka huu Mwamposa na wenzake saba waliokuwa wanashikiliwa na polisi kutokana na tukio hilo waliachiwa kwa dhamana.
“UPINZANI WABUNGE KUNA NDOA ZA JINSIA MOJA, TULIENI NACHOMA SINDANO”