Wiki iliyopita katika mitandao ya kijamii kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu mtoto aliyetengeneza jezi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi kwa mfuko wa rambo na kuivaa. Kwa mapenzi ya dogo kwa Lionel Messi alitengeneza jezi ya Argentina yenye jina na namba ya Messi.
Picha ya dogo huyo mwenye umri wa miaka mitano iliingia kwenye headlines katikati ya mwezi January na baaadhi ya vyombo vya habari kuanza kumtafuta, dogo anaitwa Murtaza Ahmadi anatokea Afghanistan maeneo ya vijijini, January 31 stori kutoka 101greatgoals.com inatajwa kuwa taarifa zimemfikia Lionel Messi na anajiandaa kukutana na dogo huyo.
Stori hizo zinapata nguvu baada ya mtandao wa Argentine Sports website TYC kuandika pia. Lionel Messi anatajwa kuamua kukutana na dogo, lakini bado haijajulikana tarehe wala muda.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.