Usiku wa kuamkia Jumatatu wezi wanaodhaniwa kuwa mashabiki wa klabu ya Borrusia Dortmund wamemfanyia kitu mbaya mshambuliaji wa timu hiyo Robert Lewandoski kwa kuiba matairi yote ya gari linalomilikiwa na staa huyu.
Ni gari aina ya Porsche Cayenne lililokua limepaki nje ya nyumba ya mshambuliaji huyo huko Ujerumani, wezi waliiba matairi yote na kuliacha juu ya mawe.
Kwa mujibu wa gazeti la Bild, sasa itamgharimu Lewandowski kiasi cha €2,500 kuweza kulifanya gari lake litembee tena ambapo inasemekana huenda mashabiki wa Dortmund wameamua kumfanyizia hivi baada ya kukerwa na staa huyu kusaini pre-contract kwenye kuichezea Bayern Munich.