Kama kuna vitu vinayakimbiza maisha kwenye kasi ya ajabu, basi teknolojia nayo imo… uliipata ile ya Lexus iliyotengenezwa kwa mabox, ikafungwa mota alafu ikaingia barabarani na kutembea kama gari tulizozoea?
Sasahivi nimekutana na hii ambayo jamaa wamekaa zao chimbo kubuni tu kitu tofauti… kilichobuniwa ni matairi yaliyotengenezwa kwa barafu, ubunifu umefanyika London Uingereza na kampuni ya Hamilton Ice Sculptors ambao ni mabingwa wa kutengeneza vitu mbalimbali kwa kutumia barafu.
Unaambiwa gari ambalo lilifungwa matairi hayo kwa majaribio na lenyewe liligandishwa kwa muda wa kama siku tano hivi kabla ya kufungwa tairi hizo.
Iko hapa na videoya ubunifu huu wa nguvu mtu wangu, Lexus na tairi zake za barafu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.