Leo August 30, 2017 Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob amefanya mkutano wa hadhara kuzungumza na Wamachinga uliofanyika Makutano ya Ubungo Mataa kuzuia vyombo vya ulinzi na usalama kuwaondoa kwa nguvu.
Aidha, katika mkutano huo uliokuwa na dhamira ya kuzuia vyombo vya Ulinzi na Usalama kuwaondosha kwa nguvu Wamachinga baada ya kulalamikiwa na Mkandarasi wa FLYOVER UBUNGO akidai wamezagaa ovyo katika maeneo hayo hivyo kukwamisha Ujenzi wa Mradi ikiwemo kukosa eneo la kuweka vifaa vyao.
Meya Jacob amewaomba Wamachinga kupisha kwa amani ikiwa ni ishara ya kumuunga mkono katika jitihada za kushughulikiwa kero zao bila Jeshi la Polisi kuwapiga Mabomu akiwaruhusu kufanya popote barabarani nje ya eneo la Mradi.
ULIPITWA? Maamuzi ya Meya wa Ubungo kwa walioongeza ushuru Kituo cha Simu 2000