Habari ya kimataifa leo February 19, 2018 ni pamoja na Bunge la nchini Iceland siku za hizi karibuni limependekeza sheria mpya ya kupiga marufuku kutahiri watoto wa kiume nchini humo.
Jambo hili limepingwa na kulaaniwa vikali na viongozi wa kidini nchini humo ambao wamesema viongozi hao wanafanya maamuzi ambayo yako kinyume na matakwa ya kitibabu na yanakiuka haki za mtoto.
Rasimu ya sheria hiyo inaeleza kuwa itamweka gerezani kwa miaka sita mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kumtahiri mtoto yeyote.
Hata hivyo viongozi wa Kiyahudi na Waislam wameita muswada huo kuwa shambulio la uhuru wa kidini.
Sheria hiyo ikipitishwa, Iceland itakuwa nchi ya kwanza ya Ulaya kupiga marufuku utaratibu wa kutahiri watoto.
Maamuzi ya Mahakama Dodoma kuhusu Kesi ya NABII TITO
Mwanamitindo maarufu Nchini aliyealikwa Ikulu ya Uingereza