June 3, 2018 Naibu Spika Dr Tulia Ackson kupitia taasisi yake ya Tulia Trust aliungana na waislamu wote mkoani Mbeya kwa ajili ya kushiriki futari iliyoandaliwa na taasisi hiyo lengo likiwa ni kuimarisha uhusiano wa kijamii. Hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Mtenda Sunset iliwaunganisha pia waumini wa imani mbalimbali wakiwemo machifu na viongozi wa dini za kikristo.
Dr Tulia alisema >>> “Ni vizuri sisi kama jamii kuungana kwa pamoja na tumuombe M/Mungu aendelee kutujaalia baraka zake ili tuendelee kulifanya jambo kama hili kila wakati. Hii ni fursa kwa sisi kama jamii kukaa pamoja tukiwa na imani tofauti, utaona Maaskofu wako hapa, Machivu, Mashehe na vijana wako hapa kwamaana hiyo hii inatuonesha sisi watanzania ni wamoja na tunaweza kukaa pamoja”
KWA WANAFUNZI WA DIPLOMA, TAARIFA MPYA KUHUSU KUCHUKUA MKOPO