Ununuzi wa bilionea wa Uingereza Jim Ratcliffe wa asilimia 25 ya hisa katika Manchester United hatimaye umeidhinishwa na Ligi Kuu ya Uingereza.
Update kutoka kweneye Tume ya Usalama na Ubadilishanaji wa Fedha ya Marekani (SEC) Jumatatu jioni ilifichua uamuzi wa Ligi Kuu ya kutoa mwanga wa kijani kwa uwekezaji huo wa Ratcliffe.
United bado inasubiri idhini ya Chama cha Soka kwa ajili ya mkataba huo, ambao Ratcliffe alisema unaweza kukamilika katikati ya Februari na utampa udhibiti wa uendeshaji wa soka Old Trafford.
Inafahamika kwamba kibali cha Ligi Kuu ya Uingereza kinategemea mkataba huo kukamilika, na kwa hivyo ligi haitathibitisha kuwa imetoa kibali hadi au isipokuwa hilo lifanyike.