Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema kuwa sekta ya mawasiliano nchini imekuwa kwa kasi ambapo mpaka kufikia hivi sasa kuna jumla ya Line za simu zilizo “active” Milioni 72 kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na TCRA hivi karibuni ikiwa ni ongezeko kubwa ukilinganisha na mwaka 2002 ambapo kulikuwa na jumla ya line za simu Milioni 51.
Waziri Nape ameyasema hayo leo April 25 jijini Dodoma mbele ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango katika halfa ya Uzinduzi wa Jengo la UCSAF ambao ni mfuko wa wa Mawasiliano kwa wote.
“Mwaka 2002 kulikuwa na jumlq ya line za simu milioni 51, Twakwimu mpya zilizotolewa mwaka huu na TCRA zimeonyesha tuna line za simu zilizo active Milioni 72, ambapo pia jumla ya Line Milioni 32 zimeunganishwa na huduma za kifedha ikiwa ni ongezeko kubwa ukilinganisha na mwaka 2020 ambapo jumla ya line za simu Milioni 5 pekee zilikuwa zimeunganishwa na huduma za kifedha” amesema Waziri Nape.