Nahodha wa Inter Miami Lionel Messi huenda akakabiliwa na adhabu baada ya kitendo chake baada ya klabu hiyo kushinda 2-0 dhidi ya New York Red Bulls.
Lionel Messi alifunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 wa Inter Miami dhidi ya New York Red Bulls katika mchezo wake wa kwanza wa MLS lakini supastaa huyo wa Argentina alikataa kuzungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo kumalizika.
Uamuzi wa Messi wa kutozungumza na wanahabari ni ukiukaji wa kanuni za MLS baada ya msemaji wa Miami Molly Dreska kusema baada ya mechi hiyo kuwa Messi hakutolewa kwa waandishi.
Dan Courtemanche, makamu wa rais wa mawasiliano wa MLS, alisema kabla ya mchezo kwamba Messi, kama wachezaji wote, alitakiwa kupatikana kwa vyombo vya habari baada ya michezo.
Haijulikani ni adhabu gani inaweza kuwa na inabakia kuonekana ikiwa MLS inaona hatua zake zinastahili kuwekewa vikwazo hata kidogo.