Mchezaji nguli wa Argentina Lionel Messi atajiunga na Inter Miami ya Marekani baada ya kuondoka kaytika klabu ya Ufaransa Paris St-Germain na anatazamiwa kukataa ofa nono zaidi kutoka kwa klabu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia.
Watendaji kutoka Al Hilal walisafiri kwa ndege kwenda Paris kukutana na baba yake Messi na wakala Jorge ili kujadili uwezekano wa uhamisho wa Euro milioni 400.
Barcelona pia iliaminika kuwa na nia ya kumrejesha Messi katika klabu hiyo lakini vikwazo vya Financial Fair Play vilifanya jambo hilo kuwa lisilowezekana. Klabu hiyo pia inatumia pesa nyingi katika ujenzi wa uwanja wao wa Camp Nou.
Akiwa PSG, Messi alishinda Ligue 1 katika misimu yake yote miwili katika klabu hiyo lakini akashindwa katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.
Alifunga mabao 32 katika mechi 75 akiwa na Parisians – na alimaliza msimu huu akiwa na mabao 16 na asisti 16 kwenye Ligue 1.
Hii ni mara ya kwanza kwa nyota wa Barcelona Messi kucheza nje ya bara Uropa.
Alitaka kubaki Ulaya kwa msimu mwingine lakini, baada ya kutopokea ofa za kuridhisha, alikuwa na chaguo moja kwa moja kati ya Inter Miami au Al-Hilal.
Alipendekezwa sana kupendelea kuhamia Saudi Arabia, ambapo angejiunga na Cristiano Ronaldo na Karim Benzema kwenye ligi kwa makubaliano ambayo hayangeweza kuafikiwa kifedha.