Taarifa kutoka ofisi ya Bunge July 26, 2017 zilieleza kuwa Spika Job Ndugai ameridhia kufutwa uanachama kwa Wabunge nane wa CUF waliosimamishwa kutokana na makosa mbalimbali ya kinidhamu hivyo nafasi zao ziko wazi.
Leo July 27, 2017 Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba amekutana na Waandishi wa Habari kuizungumzia issue hiyo.
“Tulifanya uamuzi wa kuwafukuza uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum na tulifanya kwa sababu wamekuwa wanakihujumu Chama. Katiba inasema Msemaji Mkuu wa mambo ya CUF ni Mwenyekiti wa Taifa, wao wakajenga mazingira kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe awe Msemaji wa Chama cha CUF.” – Prof. Lipumba.
ULIPITWA? CUF ya Prof. Lipumba vs Maalim Seif walivyokutana Mahakamani…PLAY kwenye video hii kutazama kila kitu!!
PLAY kwenye VIDEO hii kushuhudia Prof. Lipumba akifunguka na kujibu tuhuma alizotoa Maalim Seif!!!