Chama cha wananchi CUF kimezindua rasmi kampeni zake katika viwanja vya Sabasaba mkoani Mtwara, ambapo mgombea wa Urais kupitia chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba, amesema kama atachaguliwa atazingatia demokrasia na kuwa Rais wa kwanza atakayepata tuzo za MO Ibrahim.
Profesa Lipumba amesema kuwa tuzo hizo, hutolewa kwa Marais ambao wanazingatia demokrasia na kuheshimu haki za binadamu na kudai kuwa hilo litakuwa lengo lake.
”Mikoa ya kusini ina bahati ya kuwa na fukwe kubwa, Mgombea mwenza wangu ni mwekezaji katika Hoteli za kitalii amepita Lindi na Mtwara anaiona Bahari, anaioina fursa ya kuweza kutumia kuwa na biashara kubwa za kitalii” Profesa Lipumba
”Kama kuna watu wana haki ya kuikataa CCM basi ni watu wa Kusini, mna Bahari lakini uvuvi unaofanyika ni uvuvi ulioduni na usio tumia vyombo vya kisasa, utastaajabu Tanzania tuna Bahari kubwa lakini eti tunavua Samaki wengi kwenye maji baridi kuliko baharini” Prof. Lipumba