Wapo wanawake ambao ni wajawazito na wanatumia vilevi, Mbunge Kidawa Hamid Salehe akauliza swali kuhusu athari za vilevi kwa mtoto aliye tumboni.
Naibu Waziri Steven Kebwe akatoa haya majibu >>> “Dawa za kulevya na vileo vikali zina madhara kwenye mfumo wa mwili wa binadamu ikiwemo mtoto ambaye hajazaliwa… Madhara yanayoweza kujitokeza kwa motto ni pamoja na kupunguza ukuaji wa Ubongo, kuathirika kwa mfumo wa uzazi pamoja na kuzaa watoto wenye mtindio wa Ubongo, kuharibika kwa mimba sambamba na kuzaa watoto njiti…
Mtoto akizaliwa uwezo wa kujifunza unakuwa mdogo, anakuwa na tabia ya kutotulia mahali pamoja, kuwa na wasiwasi na msongo mkubwa wa mawazo nap engine motto akafia tumboni.
Kuna uwezekano pia mama akaambukizwa magonjwa ya zinaa, au kusababisha mtoto kuzaliwa na ngozi kama ya mzee”>>> Naibu Waziri wa Afya na ustawi wa jamii, Dk. Steven Kebwe.
Swali na majibu ya Naibu Waziri utaweza kuyasikiliza kwenye hii sauti hapa.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.