June 29 2016 Mbunge wa Singida Mashariki ‘CHADEMA’ alisweka rumande katika kituo kikuu cha polisi, Dar es salaam kwa madai ya kutoa kauli ya uchochezi kwa kumuita Rais wa nchi ‘dikteta uchwara’.
Inadaiwa kwamba Tundu Lissu alitoa kauli hiyo ya uchochezi nje ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kesi yake nyingine inayomhusisha yeye na wenzake watatu wanaotuhumiwa kwa kauli za uchochezi kupitia gazeti la mawio kwa kuandika uchaguzi wa Zanzibar ungesababisha machafuko.
Leo June 30 2016 Tundu Lissu amesomewa shitaka lake la kutoa maneno ya uchochezi nje ya mahakama ya hakimu mkazi kisutu June 28 2016 kinyume cha kifungu namba 32 ya sheria ya magazeti. Lissu amekana shtaka hilo na ameachiwa kwa dhamana na hatotakiwa kusafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama.
Tundu Lissu anatetewa na mawakili 11 akiwemo John Mallya na Peter kibatara wakati upande wa Jamhuri una mawakili watatu wanaosimamia kesi hiyo, kesi hiyo itasikilizwa August 02 2016.
ULIKOSA HII YA TUNDU LISSU KUHOJIWA NA POLISI KWA MASAA MATATU? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE