Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (CHADEMA), Tundu Lissu amezungumzia kesi takribani sita za Jinai zinazomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo miongoni mwa kesi yake itatajwa August 26, 2020 siku ambayo ni Uzinduzi wa Kampeni za Vyama vya Kisiasa nchini Tanzania.
“Je utaenda Kisutu au lah? Nitaenda Kisutu lakini nitaenda Kisutu baada ya kuhakikisha kwamba lile tendo la Kikatiba (Uchaguzi Mkuu) linalokuja mara moja kila baada ya miaka 5” Lissu
“Nimelitekeleza kwa ukamilifu wake.Kesi za jinai zilizopo mahakamani kama zimeweza kusimama hazijaendelea kwa miaka 3, haitashindikana kuzisogeza mbele kwa miezi miwili,” Lissu