August 5 2016 Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu alifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu, Dar es salaam na kusomewa mashitaka matatu likiwemo la kutoa kauli za uchochezi nje ya mahakama hiyo August 2 2016 dhidi ya Serikali iliyopo madarakani.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo Lissu ambaye alikuwa akijitetea mwenyewe kufuatia mawakili wa serikali kupinga uhalali wa wakili Peter Kibatala aliyeteuliwa kumtetea kuwekewa pingamizi lakuwa na yeye ni mmoja wa mashahidi wa tuhuma hizo Lissu alikubali mashitaka yote kuwa ni ya kweli isipokuwa hakuvunja sheria yoyote.
Baada ya kusikiliza pande zote za mashitaka na mshitakiwa ndipo hakimu mfawidhi Cyprian Mkea akatatoa maamuzi ya kumtaka Lissu kujidhamini mwenyewe kwa malipo ya shilingi milioni 10 ambazo alizilipa na kuachiwa huru huku tarehe ya kusomewa shitaka ikitajwa kuwa ni August 19 2016.
Hizi nii baadhi ya Updates nilizokuwa nikikusogezea kupitia account yangu ya Twitter..
Mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu akifikishwa ktk mahakama ya kisutu baada ya kudaiwa kutoa kauli za uchochezi pic.twitter.com/pp5HPkVMUH
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#MillardAyoUPDATES Mahakama ya kisutu imetoa dakika 20 kwa mawakili wa serikali kujadili upya shitaka la Tundu Lissu pic.twitter.com/JpaOdNFMDs
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#MillardAyoLiVeUPDATES Baada ya mawakili wa serikali kupinga Tundu Lissu kutetewa na wakili Peter Kibatala, Lissu ameamua kujitetea mwenyewe
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#MillardAyoUPDATES Mahakama itasikiliza tena shitaka la Lissu 19 Aug, anakabiliwa na mashitaka matatu ikiwemo kutoa maneno ya uchochezi tar.
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
Upande wa serikali unaiomba Mahakama iendelee kumshikilia Lissu kwa wiki 2 kupisha upelelezi sababu ikimuachia anaweza kurudia kosa hilohilo
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
#MillardAyoUPDATES Mahakama ya Kisutu Dar es salaam imemtaka Tundu Lissu kujidhamini mwenyewe kwa malipo ya milioni 10, kazilipa tayari.
— millardayo (@millardayo) August 5, 2016
ULIIKOSA HII KAULI YA TUNDU LIZZU BAADA YA KUTOKA MAHAKAMANI