Serikali ya Lithuania inasema imeamua kufunga vivuko viwili kati ya sita vya nchi hiyo na Belarus kutokana na “hali ya kijiografia”, wiki kadhaa baada ya wanajeshi wa Kikundi cha Wagner wa Urusi kuwasili nchini.
Lithuania ilitangaza kuwa vituo viwili vya kuvuka vijijini ambavyo havitumiwi na magari ya kibiashara vitafungwa kuanzia Ijumaa.
Nchi jirani ya Poland wiki iliyopita ilitangaza mipango ya kuhamisha wanajeshi 10,000 wa ziada kwenye mpaka wa Belarus katika hatua ya kuulinda dhidi ya kile ilichokitaja kuwa tishio kwenye ubavu wa mashariki wa NATO.
Tazama pia….