Matokeo ya awali ya urais nchini Marekani kati ya, Donald Trump na hasimu wake wa Democrat, Joe Biden yanaonesha mchuano kuwa mkali katika majimbo kadhaa.
Donald Trump anaongoza katika jimbo la Florida kwa karibu kura zote zilizohesabiwa.
Lakini majimbo mengine ya Georgia, Pennsylvania, Wisconsin, Michigan, Arizona, Ohio, Texas, na North Carolina chochote kinatarajiwa.
Zaidi ya watu Milioni 100 walikwisha piga kura zao za mapema, Marekani inaonekana kuwa idadi ya waliojitokeza zaidi katika karne.
Udhibiti wa Congress pia uko hatarini pamoja na Ikulu ya White House, Republican wanawania kupata idadi kubwa ya viti vya Seneti.