Mmiliki wa Liverpool Fenway Sports Group (FSG) anatazamiwa kumteua mkurugenzi wa ufundi wa Benfica Pedro Marques, kwa mujibu wa The Athletic.
Kampuni hiyo yenye maskani yake Boston itaajiri Marques kwa muundo wao mpya wa soka badala ya Liverpool.
Marques alitumia miaka sita kufanya kazi Sporting Lisbon kabla ya kujiunga na Manchester City mnamo 2010 kama mkufunzi. Alirudi Ureno kama mkurugenzi wa kiufundi wa vijana wa Benfica baada ya miaka minane.
Michael Edwards amerejea FSG kama Mkurugenzi Mtendaji wa kandanda huku Richard Hughes akiwa mkurugenzi mpya wa michezo wa Liverpool kuanzia mwisho wa msimu huu.