Giorgi Mamadashvili amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Arne Slot kama meneja wa Liverpool – lakini kipa huyo atasalia na Valencia hadi msimu ujao wa joto.
Liverpool wamekubali dili la kumsaini mchezaji huyo wa kimataifa wa Georgia kwa £25m pamoja na £4m za nyongeza.
Mamadashvili kisha atahamia Anfield mwaka wa 2025, ambako kuna uwezekano mkubwa atashindana na Alisson na Caoimhin Kelleher kuwania jezi nambari 1.
Liverpool kwa sasa ina makipa watatu katika kikosi cha wakubwa – Marcelo Pitaluga, Alisson na Kelleher – ambao wote wamebakiza miaka miwili kwenye mikataba yao.
Alisson ana chaguo la kuongeza mwaka kwenye mkataba wake.