Liverpool wamekubali ada ya uhamisho wa rekodi ya Uingereza ya £111m na Brighton kwa ajili ya kiungo Moises Caicedo.
Baada ya Brighton kukataa ofa nyingi kutoka kwa Chelsea, bado haijafahamika iwapo The Blues sasa watafikia kiasi hicho.
Brighton walikuwa wameweka ada ya zaidi ya £100m kwa Caicedo na walisema wanahisi hakuna mtu angeifikia.
Hata hivyo, Liverpool sasa wamefanya hivyo, jambo ambalo linamwacha mchezaji huyo wa kimataifa wa Ecuador mwenye umri wa miaka 21 huru kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.
Liverpool ilipoteza viungo Jordan Henderson na Fabinho kwenye Ligi ya Pro ya Saudi mwezi uliopita lakini ikamsajili mchezaji mwenza wa Brighton Alexis Mac Allister mwezi Juni kwa £35m.
Ada iliyokubaliwa kwa Caicedo inazidi pauni milioni 107 ambazo Chelsea walilipa kwa kiungo wa Argentina Enzo Fernandez mapema mwaka huu.
Caicedo alijiunga na Brighton akitokea Independiente del Valle ya Ecuador kwa £4m Februari 2021, huku kipengele cha mauzo cha 20% kikijumuishwa katika mkataba huo.
Hakucheza mechi yake ya kwanza Ligi Kuu hadi Aprili 2022.