Klabu ya Liverpool hii leo imetangaza kuingia mkataba na kmapuni ya kutengeneza vifaa vya michezo ya Marekani ya New Balance mkataba ambao unaweka rekodi ya kuwa mkataba mnono kuliko yote katika historia ya klabu hiyo .
Kampuni hii ambayo makao makuu yake yako huko Boston nchini Marekani inachukua nafasi ya kampuni ya Warrior ambayo imekuwa ikidhamini Liverpool tangu miaka mitatu iliyopita na itaanza rasmi kazi na Liverpool katika msimu wa mwaka 2015/2016.
Thamani ya mkataba ambao New Balance imeingia na Liverpool itakuwa paundi milioni 25 kwa mwaka huku kampuni hiyo ikisimamia utengenezaji wa jezi na vifaa vyote vya maeozi pamoja na nenmbo yake kuonekana kwenye jezi ya timu hiyo.
New Balance ndio kampuni mama ya Warrior ambao ndio wadhamini wa sasa wa Liverpool kwa upande wa utengenezaji wa jezi zake na mafanikio yaliyopatikana katika miaka mitatu ya mkataba na Liverpoool umeishawishi kampuni ya New Balance kuingia kwenye soko la mchezo wa soka .