Stori kutoka Uhispania leo May 15, 2018 Bunge la Catalonia limemchagua Quim Torra kuwa rais wao mpya. Jimbo la Catalonia linapania kujitenga na kujitawala kutoka kwa Uhispania.
Kuchaguliwa kwa Torra kunafikisha ukingoni miezi saba ya utawala wa dharura wa moja kwa moja wa serikali kuu ya Uhispania uliotangazwa mwaka jana na kuanzisha tena harakati za kujitenga na Uhispania.
Bunge hilo la Catalonia lililogawanyika pakubwa limepiga kura 66 dhidi ya 65 kumchagua Torra ambaye aliidhinishwa na aliyekuwa rais wa jimbo Carles Puigdemont ambaye yuko Ujerumani alikokamatwa kufuatia waranti iliyotolewa na mahakama ya juu ya Uhispania dhidi ya kiongozi huyo wa Catalonia anayetakiwa kujibu mashtaka ya uhaini na ubadhirifu wa mali ya umma.