Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari vimechapisha taarifa zinazosema kwamba Tanzania imekumbwa na njaa. Leo January 11 2017 Rais Dkt. John Magufuli alipokuwa kwenye ziara yake mkoani Simiyu amezungumza kuhusu suala hilo, hizi hapa ni baadhi ya kauli zake….
'Nafahamu kuna maeneo ya TZ mvua zimechelewa, tusilime mahindi yanahitaji maji mengi, lima mtama, ulezi na viazi'-Rais Magufuli #ZiaraSIMIYU
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
'Wapo wanasiasa wachache ambao 'bure' haijawatoka kichwani kwao, kila kitu kikitokea Serikali fanya hili'-Rais Magufuli #ZiaraSIMIYU
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
'Serikali ninayoiongoza mimi haitafanya kila kitu, mlinichagua niseme ukweli, kwa hiyo niwaombe watu wafanye kazi-Rais Magufuli #ZiaraSIMIYU
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
'Nimepita sehemu mtu amelima mahindi yamekauka na ni kando ya ziwa, anashindwa kuchukua maji kumwagilia, anataka serikali ilete chakula'-JPM
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
'Wako wafanyabiashara wanatumia magazeti kusema kuna njaa, wanataka wasamehewe kodi ya mahindi yao kutoka Brazil, wayauze TZ ikose kodi-JPM
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
'Anayejua kuna njaa ni Rais wala sio gazeti fulani, mimi ndio nimepewa dhamana ya kuongoza watanzania wote'-Rais Magufuli #ZiaraSIMIYU
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
'Nilimsikia mtu mmoja huko Mvomero naye alilipwa fedha, akazungumza kuna ng'ombe 17,000 wamekufa eti wamekosa maji, majani'-JPM #ZiaraSIMIYU
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
'Watatumika lakini sitawasikiliza, wataandika wala sisikii, nataka Watanzania wafanye kazi'-Rais Magufuli #ZiaraSIMIYU
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
'Mwaka jana wabunge walizungumza chakula ni kingi kwa hiyo wakauze Uganda, niliwazuia lakini ni haohao leo wanasema waletewe chakula'-JPM
— millardayo (@millardayo) January 11, 2017
VIDEO: Rais Magufuli alivyotembelea shule ya msingi aliyosomea Chato, Bonyeza play hapa chini kutazama