Kesi iliyofunguliwa na Bodi ya wadhamini CUF dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) George Masaju, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, Profesa Ibrahimu Lipumba na wanachama 11 wa chama hicho imesikilizwa leo December 14 2016 mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
Kesi hiyo iliposikilizwa December 6 wakili wa bodi ya wadhamini CUF, Juma Nassoro aliomba Jaji anayesimamia kesi, Jaji Kihiyo ajiondoe kwenye kesi hiyo.
Wakili Nassoro alitaja hoja kuu mbili, ya kwanza alisema inajengwa na kesi hiyo wakati ilipotajwa Novemba 11, mwaka huu ambapo Jaji Kihiyo aliibua hoja iliyohusu uhalali wa wadhamini ambayo ilikuwa na muelekeo wa kuwaonyesha wadaiwa nini wafanye.Aidha hoja nyingine ni kauli iliyotolewa na Jaji huyo kwamba shauri hilo limefunguliwa kwa haraka haraka.
Leo December 14 2016 jaji wa mahakama Kuu ya Tanzania, Sakieti Kihiyo ametoa uamuzi kuhusu ombi hilo la bodi ya wadhamini CUF ambapo amesema amezingatia hoja za mawakili wa pande zote na vilevile kupitia barua iliyoandikwa na mwombaji ya tarehe 16/11/2016.
Jaji amesema madai ya waombaji hayana ukweli hivyo hakuna sababu ya msingi ya yeye kujitoa kusikiliza shauri hilo kwa kuwa maombi ya yeye kujitoa katika shauri hilo hayana msingi hivyo anayakataa
ULIKOSA? Jaji anayesikiliza kesi ya Lipumba, Bodi ya wadhamini CUF ilivyotaka ajitoe, Bonyeza play kuatazama hapa chini