Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Aikael Mbowe amezungumza na waandishi wa habari nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya baada ya kumaliza kusikiliza kesi ya Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi
Mbowe amesema amesikitishwa na namna inavyoendeshwa kesi ya ‘Sugu’ na Katibu CHADEMA kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga iliyoahirishwa leo na kuzitaka mamlaka husika zinazosimamia sheria nchini kujiangalia vizuri katika utendaji kazi.
“Tumesikitishwa na suala hili jinsi linavyoshughulikiwa, sipendi kuingilia uhuru wa Mahakama, mienendo ya kimahakama lakini mimi kama raia na kiongozi nafikili vyombo vinavyostahili kutoa haki kwa wananchi vinawajibu wa kujiangalia vizuri,”- Mbowe
“Mahakimu, Majaji, Mawakili wa Serikali pamoja na Askari wenyewe pia binadamu haina maana kwamba wao hawawezi kufanya makosa wao ni binadamu kama walivyo wengine”, Mbowe.
KESI YA SUGU: SUGU AMKATAA HAKIMU WA KESI YAO, MAWAKILI WAJITOA