Wiki tatu za kukataza watu kutoka nje nchini India zilizowekwa tangu Machi 25 zilitarajiwa kumalizika usiku wa manane leo lakini waziri mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi amesema leo kuwa hatua za kuzuwia watu kutoka nje nchini humo, zimesogezwa mbele.
Watu wapatao bilioni 1.3 wataendelea kubaki majumbani mwao hadi Mei 3 licha ya malalamiko kutoka kwa mamilioni ya watu masikini ambao wamebaki karibu bila msaada wowote wakati ajira na mapato yakitoweka.
Modi amesema kuwa kwa mtazamo wa kiuchumi, India imepata pigo kubwa, lakini maisha ya watu wa India yana thamani kubwa zaidi lakini inawezekana kulegeza vizuwizi kuanzia Aprili 20.
Hadi sasa nchi ya India ina visa 10,000 vya maambukizi ya virusi vya corona na vifo 339.