Leo December 21, 2017 Uongozi wa Kiwanda cha Urafiki Textile kupitia kwa Meneja wake Shadrack Nkelebe umetoa siku 14 kwa wapangaji wake kulipa malimbikizo ya pango la nyumba vinginevyo watatolewa bila kujali hadhi zao katika nyumba hizo.
“Tumekuwa na shida ya muda mrefu ambapo watu wanaona mali za seikali zinaweza kutumika ovyo hazina mwenyewe, kuna suala la wapangaji ambao tunao muda mrefu, wengine wamekuwa wadaiwa sugu, ambao wanaona ni shamba la bibi, naomba niwaambie bibi ameshakufa,” – Nkelebe
Kampuni ya Udalali ya Yono imesema muda huo ukiisha, watapiga mnada mali walizozikamata ili kufidia deni. Wadaiwa hao sugu ni takribani 160
AHADI YA TANESCO KUHUSU KUKATIKA KWA UMEME MARA KWA MARA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA