Kwenye post hii ni Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anaongea kuhusu hali ya kiafya ya Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.
Mbowe amesema mashine zilizokua zinamsaidia kuimarisha figo zake zimeondolewa, viungo vyake vyote ni timamu… hatumii tena mirija kula chakula na sasa anakula chakula chake anachokitaka yeye mwenyewe ambapo pia juzi kwa mara ya kwanza alikaa mwenyewe, kwa sasa anatembea kwenye Wheel chair.
“Viungo vyake vyote ni timamu lakini inahitaji muda ili viimarike, vilevile weekend hii kwa mara ya kwanza ameliona jua baada ya kuwekwa kwenye Wheel chair na kutembezwa kwenye bustani ya Hospitali ya Nairobi…” tazama hii video hapa chini kufahamu zaidi
BREAKING NEWS: Tundu Lissu katolewa ICU, anahamishwa nchi… bonyeza hapa chini kupata taarifa zote mwanzo mwisho
UNATAKA KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI? …. fanya jambo moja tu rahisi… BONYEZA PAGE ZIFUATAZO ili nikutumie kila kitu kiganjani mwako >>> INSTAGRAM <<<< FACEBOOK >>>> TWITTER >>> APP MPYA YA MILLARD AYO pia bonyeza SUBSCRIBE HAPA >>> YOUTUBE