Kangi Lugola ambae ni mbunge wa Mwibara (CCM) ni miongoni mwa Wabunge wachache ambao wakisimama bungeni unaweza usiache kucheka au kumsikiliza kwa makini kutokana na aina ya uwasilishaji wake.
Huu ndio ulikua mchango wake kwenye bunge la bajeti June 20 2014 Dodoma ambapo alitumia style ya aina yake ya kuwasilisha mchango wake kwa kuchora katuni na kui-frame vizuri sana ambapo kwenye picha hiyo zinaonekana katuni sita ambazo kila moja ameipa jina lake.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB