Mshambuliaji wa Inter Milan ya Italia Romelu Lukaku ameeleza hasira zake kwa kocha wa zamani wa Chelsea Andre Villas Boas kuwa hawezi kumsamehe kwa sababu ya kumuacha katika kikosi cha UEFA Champions League 2011/12.
“Kocha (Roberto) Di Matteo aliniambia kuwa nitakuwa pamoja na timu hadi baada ya fainali, alifikiria kuwa kila mmoja anatakiwa kuja kusherehekea (Ubingwa) waliokuwa wamesimamishwa na hata ambao hawakuwa kwenye kikosi cha Champions League, namshukuru kwa hilo (Di Matteo)”-Lukaku
“Hili taji (UCL) ni moja kati ya mataji niliyokuwa nayaota, unatakiwa usherehekee Ubingwa ule ukiwa kwenye timu lakini kuna mtu mmoja ambaye alinitoa (Kikosini) kocha aliyepita (Andre Villas-Boas) sitamsamehe kamwe katika sherehe zile sikushika lile Kombe kwa vidole vyangu sababu sikuwa nimeshiriki kulitwaa”-Lukaku
Lukaku aliwasili Chelsea 2011 kwa uhamisho wa pound milioni 17 lakini hakupata nafasi chini ya kocha Andre Villas-Boas na hakumjumuisha katika kikosi cha Champions League, baadae Boas alifukuzwa na nafasi yake kurithiwa na Di Matteo ambaye alitwaa Ubingwa na kuamua kumchukua Lukaku katika sherehe za Ubingwa waliporejea London wakitokea Munich ilikopigwa fainali.