Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Msomi na Mwanamajumui wa Afrika (Pan-Africanist) Prof. Patrick Loch Otieno Lumumba, Ikulu Jijini DSM.
Dkt. Magufuli na Prof. PLO Lumumba ambaye ni raia wa Kenya wamezungumzia masuala mbalimbali yahusuyo juhudi za Afrika katika kuimarisha uchumi kwa kutumia rasilimali zake na pia wajibu wa Waafrika na viongozi wao katika kuimarisha huduma za kijamii na kukabiliana na changamoto mbalimbali.