Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ameliagiza Jeshi la Polisi Dodoma kuweka vizuizi katika maeneo yote yanayouzunguka Mkoa wa Dodoma na kuhakikisha watu waliohusika kumshambulia kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu wanakamatwa.
Agizo hilo la Waziri Nchemba limekuja baada ya watu wasiojulikana kumshambulia kwa risasi Mbunge Tundu Lissu akiwa kwenye gari lake wakati anatokea Bungeni kuelekea nyumbani kwake Area D, Dodoma.
>>>”Nimeelekeza Polisi waweke vikwazo njia zote za kutoka Dodoma, waimarishe ufuatiliaji kwa njia tofauti ili kuhakikisha wahalifu waliofanya tukio hilo wanatiwa mkononi na kufikishwa katika mkono wa sheria.” – Waziri Mwigulu.
Spika Ndugai na Ummy Mwalimu wamjulia hali Tundu Lissu
Polisi na RC Dodoma waongelea Tundu Lissu kupigwa risasi