50 Cent, Justin Bieber, Mike Tyson.. Hayo ni baadhi ya majina ya mastaa ambao walijitokeza kabisa na kusema kwamba wanaamini mkali wao Floyd Mayweather atamshinda Manny Pacquiao May 2 2015.
Mtoto wa Legend wa mchezo wa Ngumi Duniani, Muhammad Ali ambaye anaitwa Rasheda Ali amesema kura ya baba yake iko upande wa Pacquiao; “My dad is Team Pacquiao all the way!”– Rasheda Ali.

Rasheda amesema baba yake huenda akawa mmoja ya mashabiki watakaojitokeza kushuhudia mpambano huo ambao kwa Muhammad ni kama utakuwa unamkumbusha enzi zake akiwa ulingoni.