Kikao cha Bunge kimeendelea leo Dodoma, moja ya mambo yaliyochukua nafasi kubwa ni hoja ya Mbunge Magdalena Sakaya na David Kafulila ambao wote headlines zao ziko kwenye wizara ya mali asili na utalii.
“… Ni jambo la ajabu Waziri wa Maliasili na Utalii anahamisha ofisi kutoka ofisi yake anakwenda kufanya ofisi kwenye hoteli tena five star hotel inalipiwa na fedha za walipakodi, Arusha permanent room five star hotel, Dar es Salaam five star hotel.. anasafiri anakwenda Ulaya chumba kinalipiwa.. anasafiri anaenda wapi chumba kinalipiwa’
‘Haya ni matumizi mabaya ya fedha.. Waziri anafanyia press conference Serena Hotel, pale Mpingo house Wizara ya Maliasili na Utalii mbala kisasa lenye ofisi nzuri, lenye kumbi nzuri haiwezekani kufanya press conference..mpaka tukafanyie Serena hotel?..”– Magdalena
“Kitendo cha Waziri wa Maliasili kutumia leseni ya Rais kutoa Wanyama 704 wa tofauti 49 wakiwemo Twiga, Tembo na Simba huu ni ufisadi kama ufisadi wa EPA.. Huu ni ufisadi kama ESCROW.. na ufisadi mwingine na mpaka leo Serikali imekaa kimya inatupa mashaka sisi Watanzania yawezekana hali peke yake huyu”– Magdalena
Kusikiliza kilichosemwa unaweza kubonyeza play hapa chini.
David Kafulila yeye amesema ‘Kwa muda mrefu sasa zimekuwepo taarifa katika Wizara ya maliasili na Utalii kwamba leseni ya Rais imetumika, imetolewa kwa familia ya Kimarekani iweze kufanya ujangili, nasema ujangili sababu ni kinyume na utaratibu… waue Wanyama wakiwemo Tembo 704, hii taarifa ni nyeti’
‘Serikali inapaswa ije na majibu, kwanza inachafua jina la Ikulu, inachafua jina la Rais… haiwezekani leseni ya Rais ambayo katika hali ya kawaida inatumika kwa heshima kama Malkia amekuja, kama kuna kiongozi muhimu amekuja ndipo Rais anaweza kutoa oda kwamba pengine huyu kwa heshima yake……….. leseni ya Rais inatumika kufanya ujangili alafu serikali inakaa kimya, haiwezekani!! hii kitu haiwezekani!!!
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook