Leo January 14, 2018 Taarifa ambayo imeshika headlines katika vyombo vya habari vya China ni kuhusu Meli ya mafuta ambayo ilikuwa ikiteketea kusini mwa bahari ya China kwa zaidi ya wiki moja sasa, hatimaye imezama.
Meli inayofahamika kwa jina la Sanchi na meli nyingine ya mizigo ziligongana kilomita 260 nje ya Shanghai January 6, 2018 ambapo baadaye ili sombwa kutoka kusini mashariki kwenda Japan.
Maafisa wa Serikali ya Iran wamesema kuwa wahudumu wote 32, wakiwemo raia 30 wa Iran na wawili wa Bangladesh wote wamefariki.
Meli hiyo ilikuwa imebeba tani 136,000 za mafuta lakini maafisa wa serikali wanasema kuwa hakuna hatari kubwa. Meli zingine 13 na kikosi kutoka Iran wamekuwa wakishiriki katika jitihada za kuokoa licha ya kuwepo hali mbaya ya hewa.
“NILIDHANI IRINGA NI KAMA ULAYA, MSIGWA RUDI USHUGHULIKE NA MATATIZO YAKO”-MUSUKUMA