April 4 2017 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan aliwaalika nyumbani kwake timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys na kupata nao chakula cha jioni kabla ya vijana hao kuondoka Tanzania.
Mama Samia aliwaalika Serengeti Boys kwa lengo la kuwapongeza na kuwaaga kuelekea michuano ya mataifa ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 itakayofanyika Gabon, kwani Serengeti Boys wanaondoka kesho April 5 kuelekea Morocco kuweka kambi ya maandalizi ya michuano hiyo.
Makamu wa Rais Mama Samia aliwapongeza na kuwapa baraka zake vijana hao ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika michuano hiyo lakini alieleza pia watakaa kama serikali na kulifanyia kazi suala la shirikisho la soka Tanzania TFF kudaiwa na TRA lililopelekea Serengeti Boys kunyang’anywa basi na TRA leo.
ALL GOALS: Taifa Stars vs Botswana March 25 2017, Full Time 2-0