Leo October 24, 2018 Utiaji saini makubalioano ya mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji wa mafuta na gesi asilia (Production sharing agreement -PSA) baina ya serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya RAKGAS ya Ras al khaimah.
Mkataba huo unahusisha kitalu maalum kinachohusisha eneo la nchi kavu ya Zanzibar na baadhi ya eneo la Bahari yake. mikataba mingine kama hii itakayofuata itahusisha maeneo mengine ya Zanzibar ambayo yamo katika hatua za matayarisho.