Mtoto mwenye umri wa miaka 10, ameielezea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi alivyoshuhudia Baba yake wa kambo, Godfrey Samweli (Nkwabi) akimnyonga Mama yake, Bahati Hussein (ambaye kwa sasa ni marehemu).
Mtoto huyo ambaye ni Darasa la Tatu, ameyaeleza hayo wakati akitoa ushahidi mbele ya Msajili wa Mahakama, Pamela Mazengo.
Katika ushahidi wake, amedai siku ya tukio walienda kulala kati ya saa 2 au 3 usiku na baadaye usiku alishituka na kuona Mama yake akirusha rusha miguu, huku Baba yake akiwa kamkaba shingo na kumwambia asipige kelele.
“Sikupiga kelele nilinyamaza na baadae nilipitiwa na usingizi hadi asubuhi…nilimuona mama akiwa amelala kitandani na sikujua kama alikufa pale pale,” alidai mtoto huyo.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 9, 2019 kwa ajili ya kuendelea na ushahidi.
ALICHOZUNGUMZA WAZIRI KAMWELWE NA WACHIMBAJI MADINI WAKUBWA DUNIANI