Leo September 6, 2019 Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amefariki dunia. mmoja wa wanafamilia ameithibitishiakuwa Robert Mugabe amefariki dunia akiwa na miaka 95.
Mugabe alikuwa nchini Singapore akipokea matibabu kwa muda mrefu.
Ameiongoza Zimbabwe kutoka 1980 mpaka 2017, alipong’olewa madarakani na makamo wake kwa msaada wa jeshi.
Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa tayari amethibitisha kupitia mtandao wa twitter juu ya taarifa za kifo hicho.