Leo August 2, 2018 Mfanyabiashara Davis Mosha amekamatwa kwa madai ya kuwazuia askari wa Idara ya Uhamiaji kutekeleza majukumu yao.
Akizungumza na AyoTV Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Ali Mtanda amesema Mosha amewashambulia askari hao na kumnyang’anya mmoja wao simu ya mkononi baada ya kufika katika jengo la Delina lililopo Sinza Mori.
“Askari walifika kwenye majengo hayo na kujitambulisha kwa mlinzi na moja kwa moja walionyeshwa ofisi za meneja. Wakati wakifanya mazungumzo ya kikazi na meneja huyo, ghafla akatokea Mosha na kuanza kuwafokea, kisha kuwashambulia na kumnyang’anya askari mmoja simu yake.” –Mtanda