Mtoto wa kike mwenye miaka saba amelazwa katika hospitali ya kata ya Marimanti nchini Kenya baada ya kunajisiwa na baba yake kabla ya kukimbia.
Akizungumza kutoka hospitali ambako alikuwa amempaleka msichana, mama yake alisema ni bahati mbaya kwamba baba anaweza kumfanyia binti yake kitendo kiovu namna hiyo.
Alisema mumewe alikuja nyumbani jioni na kuanza kugombana juu ya mtoto wao wa mwezi mmoja akisema kuwa hakuwa wake.
Alimwaga chakula ambacho mke wake alikuwa amemtayarishia kabla ya kumshukia kwa mateka na makofi.
“Sikuweza kuvumilia hili na nililazimika kukimbilia kwenye vichaka vya karibu. Wakati huo ambao sikuwepo alianza kuwapiga watoto wengine na kumtia unajisi msichana kabla ya kukimbilia, “ alisema Mama
Ilikuwa baada ya hayo mama wa msichana alikuja na kumpeleka hospitali. Afisa wa kliniki Bernard Mwenda ambaye alimhudumia msichana alisema uchunguzi ilithibitisha msichana alibakwa.
“Msichana alikuwa na mipasuko katika sehemu zake za siri lakini tunahitaji uchunguzi zaidi ili kujua kiwango cha majeruhi yake. Tunaweza kulazimishwa kumpeleka hospitali ya rufaa ya Chuka kwa matibabu zaidi,” alisema.
Mama wa msichana pia ana wasiwasi kuwa mumewe anaweza kurudi wakati akiwa hospitalini na kuendelea kuwatenda vibaya watoto wengine wawili walioachwa nyuma.
“Ningependelea watoto kupelekwa mahali salama na polisi au hata Wasamaria wema kwa sababu anaweza kurudi na kuwatenda vibaya wengine wawili,” alisema.
Mkurugenzi wa polisi wa Tharaka wa Kusini Walter Abondo alithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa harakati za kumsaka mtuhumiwa tayari zimekwisha anza.
“Hatuwezi kurudi nyuma katika kumtafuta mtuhumiwa na tutampata popote alipojificha,” alisema.
Ambulance kubeba Mirungi Waziri Ummy atoa agizo kwa Mkurugenzi