Leo July 9,2019 Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema kuwa zaidi ya makampuni 30 yaliyokuwa yanatekeleza miradi ya maji yanatarajia kupelekwa bodi ya wakandarasi nchini ili kuyazuia kutekeleza miradi yoyote ya mji.
Ametoa kauli hiyo Mkoani Kigoma wakati wa ufunguzi wa mkutano wa saba wa mwaka wa bodi za maji za mabonde nchini ambao umeshirikisha wadau mbalimbali wa maji wenye lengo la kutunza na kuendeleza rasilimali za maji.