Unaambiwa ada mpya ya kuegesha magari Nairobi imeleta utata miongoni mwa wadau katika sekta ya daladala zao a.k.a Matatu na miji ya karibu ambapo kwa sasa shughuli zimesimama Nairobi, kuanzia uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta kupitia barabara ya jogoo, mjini na barabara kuu ya Uhuru highway inayounganisha jiji la Mombasa na miji ya Magharibi mwa nchi hiyo.
Ada hii mpya inamaanisha kwamba kila aliye na Matatu analipishwa shilingi Kenya shilingi 8,000 kwa mwezi ambayo kwa Tanzania ni zaidi ya 140,000, kiasi ambacho Madereva wanasema mapato ya 14 seater hayawezi kumudu kulipa gharama hiyo.
Wafanyabiashara ya mabasi kutoka mji wa Mombasa inamaana wao wanalipia kwa jimbo la Mombasa, Taita Taveta, Machakos na jimbo la Nairobi kwa kusimama katika miji ya Mombasa, Voi, Machakos na Nairobi.